Komenti ya CR7 yavunja rekodi

Komenti ya CR7 yavunja rekodi

Komenti ya mchezaji wa ‘klabu’ ya #AlNassr Cristiano Ronaldo akimpongeza Kylian Mbappé kupitia mtandao wa Instagram yaweka rekodi ulimwenguni kwa kupata likes nyingi.

Ujumbe huo kutoka kwa CR7 ulikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza Mbappe kusajiliwa katika ‘timu’ ya ndoto zake ‘Real Madrid’. Ujumbe umevunja rekodi kwa kupata likes zaidi ya milioni 4.

Ikumbukwe kuwa siku mbili zilizopita mchezaji wa zamani wa PSG Kylian Mbappé alitambulishwa rasmi na mabingwa wa Ligi Kuu Hispania 2023/24.

Mshambuliaji huyo ataitumikia Madrid kwa mkataba wa miaka mitano hadi 2029.

Kylian Mbappe amewahi kuzitumikia klabu mbalimbali zikiwemo ‘Monaco’, ‘Paris Saint-Germain’, na sasa ataitumikia ‘Real Madrid’


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post