Komasava Remix yafikisha views milioni 10

Komasava Remix yafikisha views milioni 10

Video ya wimbo unaoshikiria namba moja YouTube, Tanzania wa ’Komasava Remix’ umefikisha watazamaji milioni 10 ukiwa na wiki mbili tuu tangu kuachia kwake.

Wimbo huo wa nyota wa Bongo Fleva Diamond aliomshirikisha Jason Derulo, Khalil Harrison, na Chley Nkosi unazidi kuchanja mbuga baada ya kutumia lugha mbalimbali ikiwemo Kichina, Kihindi, Kifaransa na lugha nyingine.

Diamond aliiachia ‘Komasava’ kwa mara ya kwanza miezi mitatu iliyopita, akiwa amewashirikisha wakali wawili wa 'Amapiano' kutoka Afrika Kusini Khalil Harisson na Mwanadada Chley ikiwa ni Audio.

Aidha Julai 26 mwaka huu, aliachia video ya wimbo huo ambao ulikuwa remix ndani yake akionekana muimbaji huyo mashuhuri kutoka Marekani, Jason Derulo.

Mbali na hayo utakumbuka kuwa wimbo huo Agosti 6, 2024 uliingia kwenye chati za Billboard nchini Marekani, ukiwa wimbo wa kwanza kutoka Tanzania kufikia mafanikio haya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags