Komaa na vitu hivi ukihitaji Smartphone mpya

Komaa na vitu hivi ukihitaji Smartphone mpya

Eeebwana eeeh mambo vipi kijana mwenzangu! Hivi ukihitaji kununua simu mpya unafahamu vigezo vya kuangalia kabla hujafanya maamuzi? Usiogope ni mambo madogo tu chukua hii hapa.

 leo kwenye ukurasa wa smart phone nakudondoshea mambo muhimu yakuzingatia wakati unataka kununua simu mpyaa tembea kwenye vitu hivi  hapa    kwanza.

Kumbukumbu/ Memory

Chakwanza kabisa angalia memory ili ugundua matumizi ya simu yako mpya hakikisha unaangalia uwezo wa kuhifadhi je simu inanafsi kubwa ya kuhifadhi mambo? Simu za mkononi zina aina mbili za memory Random Access memory (RAM) na Read Only Memory (ROM)

Nasisitiza kuwa simu zenye RAM kubwa zitakuwa na kasi zaidi na wale walio na ROM kubwa watahifadhi vitu vingi zaidi, Mtumiaji wa wastani ili ufurahie  simu yako unapaswa kuwa na 2GB RAM na 16 GB ROM.

Bettery au betrii

Hili nalo lakuzingatiwa sana mtu wangu hakikisha unanunua simu ambayo ina uwezo wa kukaa na charji, hebu fikiria kama wewe ni mtumiaji wa simu ambaye una app nyingi kwenye simu yako unataka kuzitumia mfano kufungua videos, kucheza games je simu ambayo ina uhifadhi mdogo wa betri unafikiri hapo utatoboa? Jibu unalo mtu wangu.

Sasa fahamu kuwa matumizi makubwa kwenye mtandao hupunguza kasi ya betri  Ikiwa wewe ni  mtumiaji mkubwa, basi ni bora kwenda kwenye simu ambayo inatunza charji hiyo itakufaa zaidi kulingana na matumizi yako.

Screen Resolution

Hapa pia panakuhusu jitahidi sana kuhakikisha unaangalia suala hili kwani itakusaidia kuona ubora wa picha na video,  lakini inategemea na mahitaji yako ni jambo la kuulizia wakati unapotaka kununua simu angalau iwe na  960x1200 pixels .

Camera

Ili uweze kuifurahia zaidi simu yako suala la camera linahusika hapa wakati wa kununua simu mpya usisahau kabisa kukagua na kuulizia uwezo wa camera kwa simu utakayoihitaji kwani itakusaidia katika matumizi ya upigaji picha na video.

Kama unataka uonekane  umedamshi katika mitandao ya kijamii kama vile instagram, facebook basi usifanye uzembe wakati wa ununuzi wa smartphone yako nakufundisha jambo hapa, chukua hiyo simu kisha piga picha muulize muuzaji ina mega pixel ngapi? Ukipata majibu kama ina mega pixel kubwa basi hiyo ndiyo bora zaidi  japo kuna baadhi ya wataalamu wanapinga hilo kuwa siyo muda wote itakuwa hivyo kutokana na injini mbalimbali za simu.

Aiseee nimekuandikia hayo ambayo ndiyo muhimu zaidi lakini pia unapaswa kuangalia cost smartphone, Display, Upya na ubora wa simu yenyewe komaa na hayo mtu wangu I hope ukipita nayo utapata kilichobora zaidi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post