Kofia za kuzuia udanganyifu katika mitihani zazua mjadala mkali

Kofia za kuzuia udanganyifu katika mitihani zazua mjadala mkali

Picha za wanafunzi waliovalia "kofia za kuzuia udanganyifu" wakati wa mitihani ya chuo kikuu zimeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Ufilipino, na kuzua burudani si haba mitandaoni.

Wanafunzi katika chuo kimoja katika Jiji la Legazpi waliombwa wavae vazi ambalo lingewazuia kuchungulia majibu ya mtihani ya wenzao .

Mkufunzi wao aliiambia bbc kwamba amekuwa akitafuta "njia ya kufurahisha" kuhakikisha "uadilifu na uaminifu" katika darasa lake.

Bi Mary Joy Mandane-Ortiz, profesa wa uhandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Bicol, alisema wazo hilo lilikuwa "lenye ufanisi sana".

Baadhi walijitokeza katika ukumbi wa kufanyia mtihani kwa kutengeza kofia kwa kadibodi, maboksi, `trei’ ya kusafirisha mayai na vifaa vingine vinavyopatikana nyumbani.

kwa upande wako mwanangu sana Je ulifanya nini ili kupenyeza jibu wakati wa mtihani wako, na je ni kipi kifanyike kuzuia udanganyifu katika mitihani dondosha komenti yako hapo chini.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags