Kocha wa Al Merreikh atishwa na ubora wa Yanga

Kocha wa Al Merreikh atishwa na ubora wa Yanga

‘Kocha’ Mkuu wa ‘klabu’ Al Merreikh, Osama Nabieh amesema kuelekea mchezo wao dhidi ya ‘klabu’ ya #Yanga utakaochezwa nchini Uganda tarehe 16 mwezi huu wanatakiwa kucheza kama wanajeshi kwani Yanga iko vizuri.

Amedai kuwa ‘timu’ ya Yanga kwenye ‘mechi’ zao wameonekana wako tayari, ni ‘timu’ ambayo iko ‘fiti’ kibaya zaidi wameshinda ‘mechi’ za ‘Ligi’ na mbili za Afrika.

‘Kocha’ huyo aliendelea kudai kuwa wanalazimika kucheza ‘mechi’ za kirafiki ambazo zinaweza kuwasaidia kuwa ‘fiti’ zaidi ili kuwakabili Yanga.

Pia ameeleza ubora wa wapinzani wao kuwa mkubwa hasa eneo la kiungo, na upande wa ‘mechi’ ambazo wameziangalia kwa Yanga kama hawatakuwa na ubora wa kuwathibiti eneo hilo wanaweza kufanya makosa na kwenye ulinzi pia wapinzani wao wako vizuri.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags