Kobbie Mainoo aweka rekodi tamu Euro 2024

Kobbie Mainoo aweka rekodi tamu Euro 2024

Staa wa timu ya taifa ya England na Manchester United Kobbie Mainoo ameweka rekodi bora zaidi katika michuano ya Euro 2024, akipiga pasi sahihi nyingi kuliko wachezaji wengine wa nafasi hiyo, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kutokea tangu mwaka 1980.

Mainoo mwenye umri wa miaka 19, amekuwa katika kiwango bora katika michuano ya mwaka huu akicheza vyema kwenye eneo la kiungo la taifa hilo.

Kiungo huyu aliionesha kiwango bora katika mchezo wa hatua ya 16 dhidi ya Slovakia baada ya Trent Alexander-Arnold na Conor Gallagher wote kuonekana wanafanya vibaya katika eneo hilo.

Vile vile alifanya vizuri akitokea benchi katika michezo dhidi ya timu Serbia na Slovenia.

Mainoo ana wastani wa kupiga pasi sahihi kwa asilimia 96.38 na amepiga pasi sahihi 133 kati ya 138 alizopiga kwenye michuano hii.

Kwa mujibu wa tovuti ya Opta, Mainoo ndiye kiungo mwenye asilimia nyingi za kupiga pasi sahihi kuwahi kutokea katika michuano ya Euro tangu mwaka 1980.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post