Klopp achambua mbio za ubingwa EPL

Klopp achambua mbio za ubingwa EPL

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ni lazima washinde michezo yao yote iliyosalia kama wanataka kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England. Kocha huyo mjerumani amesema hayo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Leeds United na sasa wanazidiwa alama 3 na Mancheste City.

Liverpool imeshinda mchezo wake wa kiporo dhidi ya Leeds United jana usiku kwa ushindi wa mabao 6-0 na kukifanya kikosi hicho kutoka jiji la Liverpool kufikiha jumla ya alama 60 ikiwa ni tofauti ya alama 3 na Manchester City wanaoongoza Ligi wakiwa na alama 63 wote wakiwa wamecheza michezo sawa michezo 26.

Kuhusu mbio za ubingwa baada ya ushindi wa jana kocha Klopp amesema wanahitaji kushinda michezo yote ili kuwapiku Manchester City, 

"Ni pointi tatu tofauti kati yetu nadhani hadi wikendi, na kisha City lazima watashinda mchezo wao itakuwa pointi sita. Ikiwa tutashinda michezo yetu yote kutakuwa na nafasi. Nadhani ni bora kuwa na pengo la pointi tatu au sita kuliko kuwa na pengo la pointi 20 au 30 hivyo ni jambo la kusisimua zaidi lakini lazima tushinde mechi nyingi dhidi ya wapinzani wote wagumu na huo ni mtego kwetu. Tutajaribu." Amesema Klopp

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags