Kitayosce na Fountain Gate zafungiwa kufanya usajili

Kitayosce na Fountain Gate zafungiwa kufanya usajili

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limezingungia klabu ya Fountain Gate na Kitayosce kufanya usajili kwa wachezaji wa kimataifa, uamuzi huo umefanywa baada ya Kocha Ahmed El Faramawy Youse Mostafa Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya Klabu hizo

Pia Kitayosce,  ambayo ipo Ligi Kuu Bara na Fountain Gate inayoshiriki Ligi ya Championship zimefungiwa na TFF  kufanya usajili wa ndani.



Baada ya Soliman kushinda kesi ya kuvunjiwa mikataba, Klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya Siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hazikutekeleza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags