Kipre kinara mchezaji bora wa mwezi

Kipre kinara mchezaji bora wa mwezi

Kiungo mshambuliaji wa  ‘klabu’ ya #AzamFC, #KipreJunior, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Desemba katika ‘Ligi’ Kuu ya #NBC msimu wa 2023/24.

Kipre amewashinda Prince Dube, na Aziz Ki wa ‘klabu’ ya #Yanga, alioingia nao fainali kwenye mchakato wa Tuzo za mwezi uliofanywa na kamati ya Tuzo za #TFF.

Hata hivyo mwezi huu wa Desemba kiungo huyo ameonyesha kiwango kikubwa na kuisaidia ‘timu’ yake kupata ushindi kwenye michezo yote mitatu iliyocheza, ikiwa ni pamoja na kuhusika katika mabao manne kwa dakika 235 alizocheza.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags