Kionjo cha ngoma ya Diamond na Swae Lee

Kionjo cha ngoma ya Diamond na Swae Lee

Baada ya ‘Rapa’ kutoka Marekani #SwaeLee kuomba kufanya remix ya wimbo wa Diamond wa #Komasava’ aliomshirikisha Chley na Khalil Harrison, ili aweze kuingiza Verse (Mistari) yake, hatimaye wawili hao tayari wamefanya ‘kolabo’, hii ni baada ya ku-share kionjo cha ngoma hiyo.

Kupitia video inayoendelea kusambaa mitandaoni imemuonesha Swae Lee akiimba baadhi ya mistari iliyopo kwenye nyimbo aliyoshirikishana na Diamond.

Siku chache zilizopita Swae Lee aliomba kufanya ‘kolabo’ ya ngoma ya ‘Komasava’ kwa kuandika kwenye upande wa komenti ya posti ya Diamond akieleza “Send Me That Open Verse”.

Ombi hilo kutoka kwa ‘Rapa’ huyo linakuja baada ya Diamond ku-share video ya Swae kupitia ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akicheza wimbo wa ‘Komasava’ ambao mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 2.8 ikiwa ni mwezi mmoja tuu tangu kuachiwa kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags