Kinywaji bure kama utaacha simu kwa muhudumu

Kinywaji bure kama utaacha simu kwa muhudumu

Mgahawa maarufu kutoka nchini Italia uitwao ‘Al Condominio’ umekuja na mpango kabambe wa kuzuia wateja wake kutotumia simu wakati wa kula ambapo wametoa ofa ya kuwapatia vinywaji vya bure wateja wao endapo watazifungia simu zao kwenye droo.

Kwa mujibu wa mmiliki wa mgahawa huo aitwaye Angelo Lella aliweka wazi kuwa lengo la kutoa ofa hiyo ni kuufanya mgahawa wake kuwa wa tofauti huku akiwataka wateja kuachana na teknolojia na kuzingatia chakula pamoja na kufurahikia mandhali mazuri ya mgahawa huo.

Hata hivyo mmiliki huyo aliweka wazi kuwa muitikio umekuwa mkubwa kwa wateja wao ambapo asilimia 90 ya wateja wamechagua kuacha simu zao ili kupata mvinyo (wine) wa bure.

Siyo mara ya kwanza kwa mgahawa kutoa ofa kama hizo kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian imeripoti kuwa mgahawa mwingine kutoka nchini Italia uitwao ‘, Separè 1968’ hutoa vocha kwa wateja wanaoacha simu zao kwenye droo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags