Kim Kardashian asafiri maili 4,350 kumuona Messi na Cr7

Kim Kardashian asafiri maili 4,350 kumuona Messi na Cr7

Aliyekuwa mke wa Kanye West, Kim Kardashian ameacha maswali mengi kwa mashabiki baada ya kusafiri kwa umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kushuhudia mechi za wachezaji mashuhuri #Duniani Messi na Cristiano Ronaldo.

Kwa mujibu wa Marca news wameeleza kuwa mwanamitindo huyo amesafiri maili 4,350 kwa ajili ya kuwaridhisha watoto wake kuwaona wachezaji hao, safari hiyo haikuwa bure kwani baada ya mchezo kukamilika #Messi alipiga na picha na kumpatia mtoto wa kiume wa #Kim zawadi ya ‘Jezi’.

Safari ya #Kim haikuishia hapo kwani baada ya siku tatu aliwasili nchini Japan kutembelea jumba la makumbusho huku mwanae akiwa amevaa ‘jezi’ ya Cristiano Ronaldo ya Real Madrid akimaanisha kuwa #Ronaldo ndiyo mchezaji bora wa wakati wote.

Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Japan, Yanmar Field Nagai, mtoto huyo alibadilisha na kuvaa ‘jezi’ ya Neymer.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags