Kim Kardashian aguswa na vita ya iIrael na Palestina

Kim Kardashian aguswa na vita ya iIrael na Palestina

Baadhi ya ma-star kutoka nchini Marekani wameonekana kuguswa na vita inayoendelea kati ya Israel na Palestina huku baadhi yao wakiungua mkono nchi ya Israel, huku  kwa upande wa mwanamitindo maarufu Kim Kardashian, yeye hana upande ila amesikitishwa baada ya kuona watoto wachanga na familia zisizo na hatia zinavyoteseka.

Kim kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe kwa mara ya kwanza toka vita hiyo itokee, ujumbe wa kuwafariji uliokuwa ukieleza kuwa anawapenda sana marafiki na familia yake ya kiyahudi anawaunga mkono huku akiwatia moyo kuwa wajue hawako peke yao.

Huku akiendelea kwa kuwataka watu wanaochagua upande fulani wawe na mioyo yenye huruma kwa watoto na familia zisizo na hatia bila ya kuangalia wako upande gani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags