Kim Kardashian ageukia kwenye sheria

Kim Kardashian ageukia kwenye sheria

Mfanyabiashara na mwanamitindo maarufu Marekani amesema sasa ni wakati wake kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria.

Kim ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuchapisha picha ikimuonesha yupo darasani akiwa na madaftari huku akiandika ‘School Law’ ikiwa na maana kuwa ameamua kumalizia masomo yake ya sheria ili kutimiza ndoto zake.

Utakumbuka kuwa mwaka 2018 Kim alitangaza kujiunga na masomo ya sheria ili kutimiza ndoto yake kuwa mwanasheria ambapo alijiunga miaka minne katika kampuni ya sheria huko San Francisco California, lakini alitulia kidogo kwa muda kutokana na majukumu kuwa mengi na sasa amerudi tena kutimiza ndoto zake.

Kufuatia chapisho lake hilo katika upande wa maoni mdogo wa Kim, Khloe alimpongeza dada yake kwa kuandika “Ninakupenda mwanasheria wa MILFY” huku akiweka na emoj ya upendo.

Bilionea huyo ambaye anatambulika kupitia chapa yake ya SKIMS,pia hivi karibuni amezua taharuki kwenye mitandao ya kijamii kufuatia roboti la Telsa alilolinunua kutoka kwa Elon Musk huku wengi wakidai kuwa Kim huenda anatoka kimapenzi na roboti huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags