Kijana wa miaka 25 kuoa mwanamke wa miaka 85

Kijana wa miaka 25 kuoa mwanamke wa miaka 85

Eee bwana moja ya video ambayo inatrend katika mitandao mbalimbali ya kijamii ni ya kijana mwenye umri wa miaka 25 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Muima ambaye amezama katika penzi la Theresa bibi wa miaka 85.

Video hiyo ilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii na imekuwa gumzo kila kona kwani inaonesha namna ambayo Muima ameridhia kutoa mahari ya ng'ombe 12 ili amuoe Theresa.

Pamoja na kupishana umri wa miaka 60, wawili hawa wanapendana sana na wenyewe wanakuambia umri ni namba tu kwao.

Bibi Theresa amesema kuwa wanapendana na Muima na yupo tayari kuvaa gauni la harusi na kufunga naye pingu za maisha mazabauni.

Unaambiwa penzi lao lilianza Muima alipokwenda mjini kusoma wakati akitafuta chumba za kuishi alifanikiwa kukipata kwenye nyumba inayomilikiwa na Bibi Theresa.

Muima kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda mara baaa yay eye na rafiki yake kuamia katika nyujmba ya bibi huyo, alijikuta anampenda mama mwenye nyumba wake na kuingia katika dimbwi la mahaba mazito.

“Theresa alikuwa akinitania kwa kuniita mume wake kila ninapoingia nyumbani, mara ya kwanza aliona kama utani wa kawaida, lakini muda mwingine wakati nakosa nauli ya kwenda chuo alikuwa akinisaidia kunipatia fedha za matumizi

“Upendo huo ulinifanya nianze kumpenda Theresa taratibu, hivyo nilijikuta nampenda kuliko wanawake wote niliyowahi kuwa nao katika mahusiano,” anasema Muima






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags