Kijana bodaboda mwenye ndoto ya kutoboa kimziki

Kijana bodaboda mwenye ndoto ya kutoboa kimziki

David Samweli a.k.a Dav Sam alianza harakati zake mwaka 2019 ikiwa ndiyo mara yake ya  kwanza kuzama studio na kufanya mkwaju wake wa kwanza ambao haujatoka mpaka leo.

Nikwambie tu kijana mwenzngu, mtafutaji mwenzangu kuna usemi wa Kiswahili unasema Atafutae hachoki nah ii imedhihirika kwa kijana huyu  , hakukata tamaa mpaka mwaka huu alipoachia ngoma yake  inayotambulika kwa jina la NJOO ambayo inapatikana kwenye mtandao wa youtube.

Aidha kuingia kwenye mziki haikua kazi rahisi kwake japo kuna wasanii wengi sana bongo lakini mvuto mkubwa alipata kutoka kwa kijana mdogo mwenye machachari yake mjini Baba wa watoto wawili kutoka kwa mastaa wawili wa kike , Kusah ndio aliemvutia sana na anakubali sana kazi zake.

Hata hivyo Shughuli za bodaboda ndio anazopiga kitaa kujipatia kipato ili kupata hela ya studio na fedha kwaajili ya kujikimu na maisha ya  daily.

Sambamba na hayo  support ndiyo imekua changamoto yake kubwa sana na swala zima la management japo anafanya kazi ya  Bodaboda lakini mziki ni maisha yake pia.

Pia De Sam kama wasanii wengine wachanga anandoto pia ya kufanya ngoma na wasanii wengi wakubwa lakini kwa upande wake anavutiwa zaidi na The African princes Nandy.

 Moja ya changamoto anayopitia ni uoga aliokua nao katika kufata wasanii na kuwaambia dhumuni lake.

“Washikaji  wananiambia mimi muoga sana inabidi niende kufata Diamond nimwambie mimi naimba jambo ambalo sio rahisi ila kuna siku ntamfata tu”anasema.

Ipo wazi kwamba mziki unahitaji sapoti ya wadau De sam anasisitizia kamba anahitaji sapoti ya mtu au watu wanaoweza kumsaidia kwenye mziki asogee na anatamani siku moja aje kuwa sambamba na mziki yani ni yeye na mziki tu kula kulala mziki.

Mipango ya mwaka 2021 haikuwa mizuri japo kwa mwaka 2022 De Sama maejipanga tena kurudi studio na kufanya ngoma nyingine nyingi sana na hatoacha shughuli zake za bodaboda licha ya  nguvu nyingi atawekeza kwenye mziki.

Naam! hiyo ndiyo mipango na malengo makubwa ambayo De sam amejiwekea katika kuhakiksha anatimiza zile ndoto zake kama kijana unapaswa kusimamia malengo yako licha ya changamoto unazozipitia.

Nikuikumbushe tu kuwa muziki ni Tasnia ngumu sana kwa kipindi cha hivi karibuni na hii  hutokana na idadi kubwa sana ya wasanii wanaochipukia.

Hata hivyo ushindani kwa wasanii wakubwa ni mkubwa kuliko wengi wanavyofikiria , ukitaka kuingia kwenye mziki au msanii mchanga fanya juu chini ujue muda sahihi jitihada na kumuomba Mungu.

Ebwana eeh kwa leo ni hayo ambayo nimekuandalia kwenye makala za burudani nikukumbushe tu kujituma, kupambana na kusimamia misimamo yako ndiyo mambo makubwa yatakayo kufikisha pale unapopataka happy Friday mshikaji wangu wa faidaa!!!!!!!!!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags