Kiduku afunguka kuhusiana na pambano lake

Kiduku afunguka kuhusiana na pambano lake

Weeeuweeeh! Mzee wa show show bwana kama kawaida yake hanaga mbambamba ameweka wazi kuhusiana na pambano lake analotarajia kulifanya hivi karibuni na kuwaahidi mashabiki kutowaangusha.

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Twaha Kiduku anatarajia kupanda ulingoni September 24 mwaka huu Mkoani Mtwara kupigana na Bondia kutoka nchini Misri Abdo Khaled.

kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari Kiduku amefunguka kuwa amejipanga vizuri na ana matumaini ya kuibuka na ushindi katika Pambano hilo la kuwania mkanda wa UBO pambano ambalo litachezwa kwa raundi kumi.

Kiduku amewaomba Wadau na Mashabiki wake kuendelea kumpa support kwa kipindi chote cha maandalizi ili aweze kufanikiwa katika pambanao hilo .

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Morogoro Abdulazizi Abood ameahidi kumshika mkono kwa kipindi hiki cha maandalizi hadi siku atakapopanda ulingoni ili aweze kuliwakalisha Taifa vizuri.

Weeeeeeh! Mnasemaje anakuja kupigwa mtu kama ngoma au ndo yale yale ya ndugu yetu mtu kazi, dondosha komenti yako hapo chini mwanangui sana Kidugu atatoboaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags