Kibabage: Leo itakuwa ‘mechi’ nzuri kukutana na familia yangu

Kibabage: Leo itakuwa ‘mechi’ nzuri kukutana na familia yangu

Ikiwa leo ndiyo siku iliyosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ‘soka’ nchini ambapo ‘Ligi’ ya #NBC msimu huu inaanza rasmi ikifunguliwa na waliyo ifunga msimu uliopita, ‘klabu’ ya Yanga dhidi ya KMC watakipiga #AzamComplex Chamazi.

Licha ya hayo kuelekea mchezo huo mchezaji wa zamani wa KMC, Nickson Kibabage ambaye msimu huu yupo katika ‘klabu’ ya #Yanga ametoa maoni yake juu ya mchezo huo, amesema kuwa utakuwa mchezo mzuri sana kwani anaenda kukutana na familia yake ya zamani.

Pamoja na hayo anautambua ubora wa ‘timu’ ya Yanga tangu akiwa KMC huku akidai kuwa ataenda kuonyesha uwanjani alicho toka nacho katika ‘timu’ hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags