Kesi ya Yak Gotti na uwezekano wa kusikilizwa hadi 2027

Kesi ya Yak Gotti na uwezekano wa kusikilizwa hadi 2027

Wakati kesi ya ‘rapa’ Deamonte Kendrick, maarufu kama Yak Gotti, ikiendelea kurindima mahakamani, Mawakili wake E. Jay Abt, Douglas Weinstein, pamoja na Katie A. Hingerty siku ya jana Jumanne Machi 20 walimuomba Jaji Ural Glanville kupunguza idadi ya mashahidi wa kesi hiyo.

Kwa mujibu wa mawakili hao walifichua kuwa kesi hiyo inazaidi ya mashahidi 400 wanaotarajiwa kuitwa mahakamani huku mpaka kufikia sasa ni mashahidi 40 pekee ndio wameitwa kutoa ushahidi, jambo ambalo linaweza kusababishwa kesi hiyo kusikilizwa hadi mwaka 2027.

Aidha mawakili hao wamedai kuwa suala hilo haliwezekani na sio haki kwa washtakiwa walioko gerezani kusubiri muda wote huo mpaka mashahidi wote wakamilike.

Ikumbukwe kuwa Yak Gotti, alishitakiwa pamoja na washtakiwa wengine kadhaa katika mauaji ya Donavan Thomas mwaka 2015 na majaribio mengine ya mauaji pamoja na kuendesha genge la uhalifu liitwalo ‘Young Slime Life (YSL)’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post