Kesi ya kushindwa kulipa kodi ya Shakira yafutiliwa mbali

Kesi ya kushindwa kulipa kodi ya Shakira yafutiliwa mbali

Uchunguzi wa pili kuhusu madai ya kukwepa kodi kutoka kwa mwanamuziki wa Colombia, Shakira umefutiliwa mbali na hakimu baada ya waendesha mashitaka wa Uhispania kutaka uchunguzi na ushahidi kufanyika upya.

Mwimbaji huyo wa Colombia alikuwa anachunguzwa kwa kushindwa kulipa kodi inayogharimu kiasi cha Euro milioni 6.7 mwaka 2018 ambapo waendesha mashitaka hao walieleza kuwa Shakira alitumia mtandao wa makapuni ya nje ya nchi hiyo kukwepa kulipa kodi.

Aidha Hakimu aliamua kufuta kesi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha kumsimamisha mwanamuziki huyo kizimbani, hata hivyo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimedai kuwa endapo ushahidi utapatikana basi kesi hiyo itafunguliwa upya.

Ikumbukwe kuwa Novemba 20, 2023, Shakira mbele ya hakimu José Manuel del Amo, alikubali makosa yake sita ya kukwepa kulipa kodi kwa mwaka 2012-2014 na kukubali kulipa faini Euro milioni 7.5, lakini mwanamuziki huyo bado anakabiliwa na kesi nyingine nchini Uhispania, inayohusiana na ukwepaji wa kodi mwaka 2011.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post