Kati ya watuhumiwa wa kesi hiyo yumo anayedaiwa kuwa alihusika kutafuta silaha na usafiri, muandaaji wa tukio, watumia bunduki wawili na wawili waliokuwa wakitoa taarifa.
Majina ya watuhumiwa hao ni Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Ndimande (29), Lindani Ndimande (35), ambao ni mtu na kaka yake, Lindokuhle Thabani (30) na Mziwethemba Myeza (36).

Ikumbukwe AKA (35), aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 10, mwaka jana, alipokuwa akitembea na rafiki yake nje ya mgahawa maarufu wa Durban, Afrika Kusini.
Leave a Reply