Kenya yaongoza kwa ukarimu Afrika

Kenya yaongoza kwa ukarimu Afrika

Kwa mujibu wa shirika la kutoa misaada la kibinadamu la The Charities Aid Foundation (CAF) imetaja kuwa Kenya ndiyo nchi inayoongoza kwa ukarimu Afrika.

Ambapo imetajwa kuwa nchi hiyo inaongoza kwa ukarimu kufuatia na kuchangia misaada, kusaidia wageni na kujitolea kwa wakati pale mtu anapokuwa na uhitaji.

Kwa mujibu wa BBC imeeleza kuwa Indonesia ndilo Taifa ambalo linakisiwa kuwa na watu wakarimu zaidi duniani ikifuatiwa na Ukraine na Kenya.

Aidha uchunguzi wa mwaka huu ulikusanya maoni kutoka nchi 142 duniani kwa kuuliza maswali matatu kwa watu tofauti tofauti likiwemo je umewahi kumsaidia mgeni?. Nchi nyingine za Afrika zilizoingia katika orodha ya kumi bora ni pamoja na Liberia nafasi ya nne na Nigeria nafasi ya tisa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post