Kenya kuchunguza unyanyasaji wa kingono katika mashamba ya chai

Kenya kuchunguza unyanyasaji wa kingono katika mashamba ya chai

Bunge la Kenya limetaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono kwenye mashamba ya chai

Ilibainika  kuwa zaidi ya wanawake 70 walikuwa wamenyanyaswa na wasimamizi wao kwenye mashamba yanayoendeshwa na makampuni mawili ya Uingereza  ambayo ni Unilever na James Finlay.

Kampuni hizo zinasema kuwa zimewasimamisha kazi wasimamizi watatu wanaohusika na wao pia wameshangazwa na madai hayo.

Mbunge Beatrice Kemei, ambaye ni mwakilishi wa wanawake katika eneo linalolima chai katika kaunti ya Kericho, alisema ripoti hiyo iliangazia unyanyasaji wa kijinsia uliokithiri kwa mashirika mengi ya kimataifa ya chai yanayofanya kazi nchini humo.

Naibu Spika Gladys Shollei aliagiza kamati ya wabunge kukamilisha uchunguzi kuhusu madai hayo ndani ya wiki mbili.

Katika uchunguzi uliofanyika imebaini kuwa kuna mwanamke mmoja alisema ameambukizwa VVU na msimamizi wake, baada ya kushinikizwa kufanya naye mapenzi.

Mwanamke mwingine alisema meneja wa kitengo alimsimamisha kazi hadi akubali kufanya naye mapenzi.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post