Kendrick Lamar atajwa kuvunja rekodi ya Tupac

Kendrick Lamar atajwa kuvunja rekodi ya Tupac

‘Rapa’ kutoka Marekani Kendrick Lamar ameripotiwa kuvunja rekodi ya marehemu msanii Tupac baada ya wimbo wake wa ‘Not Like Us’ kupata streams zaidi ya milioni 647.

‘Not Like Us’ umepata mafanikio hayo na kuupiku wimbo wa 2Pac ‘Hit ‘Em Up’ kwa karibu stream milioni sita, na kuifanya ngoma ya Lamar kuwa diss track yenye stream nyingi zaidi.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Stop The Breaks’ imeeleza kuwa licha ya kuvunja rekodi hiyo pia ngoma hiyo inatajwa kuuzwa zaidi nchini Marekani kwa mwaka 2024.

Lamar aliuachia wimbo wa ‘Not Like Us’ kwa ajili ya kumchana ‘rapa’ #Drake ukiwa ni muendelezo wa bifu lao la kutoleana povu kupitia ngoma walizokuwa wakiziachia miezi michache iliyopita.

Juni, mwaka huu ‘Not Like Us’ ulikuwa umepata mauzo ya milioni mbili. Video ya muziki ya wimbo huo, inayopatikana Spotify na YouTube, inazaidi ya watazamaji milioni 800 mbali na hayo pia uliongoza katika chati za Billboard Hot 100 mara mbili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags