Keefe D adai alilipwa na P Diddy amuue Tupac

Keefe D adai alilipwa na P Diddy amuue Tupac

Mshukiwa wa mauaji ya ‘rapa’ Tupac, Keffe D” Davis, amewashangaza wengi baada ya kufunguka kueleza kuwa yeye ndiyo aliyemuua Tupac lakini ameweka wazi kuwa alitumwa kufanya mauaji hayo na P Diddy kwa kulipa dola 1 milioni.

Kwa mujibu wa The Sun inaeleza kuwa Keefe D, ambaye alifikishwa mahakamani mjini Las Vegas kuhusu mauaji hayo jana, amedai mara kadhaa kwamba Diddy alitaka amuue ‘rapa’ huyo.

Licha ya kuwa na tuhuma hizo kwa msanii huyo wa hip-hop P Diddy kuwa ni miongoni mwa watu wanaohusishwa na kifo cha Tupac ila mpaka sasa hakuna mahakama iliyothibitisha dai hilo.

Huku wawakilishi wa Diddy hawakusema lolote walipoulizwa kuhusu madai hayo lakini awali mwana hip-hop huyo alikanusha madai ya kuhusika na kifo cha Tupac.

Mauaji ya Tupac yalitokea Septemba 13,1996 akiwa Las Vegas, Nevada, US ambapo mwanzo Orlando Anderson alituhumiwa kwa kifo hicho kabla ya Keffe D.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags