Keane ataka Bruno avuliwe unahodha

Keane ataka Bruno avuliwe unahodha

Mchezaji wa zamani wa ‘klabu’ ya  #ManchesterUnited, #RoyKeane amemtaka ‘kocha’ wa ‘klabu’ hiyo Erik ten Hag amvue unahodha #BrunoFernandes  kufuatia na matatizo wanayokumbana nayo.

Keane akiwa kwenye uchambuzi wa ‘mechi’ baada ya Man United kupata kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester City amedai kuwa anawahurumia wachezaji wa Man United wanapungukiwa kila sehemu, kiufundi, kimbinu na hata kimwili hawako sawa.

Mwanasoka huyo aliendelea kwa kumzungumzia kiungo Bruno Fernandes hafai kuwa nahodha kwasababu haendani na cheo hicho alicho pewa na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo.

Alifika mbali zaidi kwa kusema ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo hayuko sawa kwasabubu mchezaji huyo anapaswa kuvuliwa unahodha japo ni uamuzi mgumu.

Hata hivyo amekiri kuwa Fernandes ni mchezaji mwenye kipaji lakini ni mtu wa kulalamika muda wote awapo katika mchezo.

Dondosha comment yako unafikiria maoni ya Keane yako sawa?
.
.
.
#MwanachiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags