Kazi ya neti kwenye ujenzi wa ghorofa

Kazi ya neti kwenye ujenzi wa ghorofa

Watu wengi wamekuwa wakiona neti ambazo huwekwa wakati wa ujenzi wa maghorofa, bila ya kufahamu umuhimu wake huku baadhi yao wakidhani huwekwa kama urembo wakati wa ujenzi wa majengo hayo.

Neti ziwekwazo kwenye ujenzi wa ghorofa linalojengwa, kwa lugha ya kingereza hufahamika kama ‘Building Safety Net au Construction Net’, neti hizo hutofautiana na zile za kuzuia mbu majumbani kwani zenyewe ni hizo ni ngumu hutengenezwa na materia aina ya ‘Heavy duty plastic’.

Mara nyingi wajenzi hutumia neti za rangi ya kijani, licha ya kuwepo za rangi nyingine kama vile nyeusi na njano. Hupendelea kijani kwa sababu ni rangi ambayo huashiria usalama, vilevile haiakisi sana joto na jua kali. Kawaida neti hizo hudumu kwa miaka miwili hadi mitatu.

Aidha sababu kubwa ya neti hizo kutumika kwenye ujenzi wa majengo hayo ni kuzuia kuanguka kwa vitu katika makazi ya watu kama vile nondo, tofari, mbao, vifusi au vitu vizito, na endapo ikitokea hivyo basi hunasa kwenye neti hizo, pia hupunguza kasi ya upepo na mvua kufikia moja kwa moja jengo, hivyo huwekwa kwa sababu ya kulinda usalama wa wafanyakazi na watembea kwa miguu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags