Kataa app hizi kwenye simu yako

Kataa app hizi kwenye simu yako

Niaje bhana! Karibu kwenye ukurasa wa Smartphone ikiwa ni Jumatano, tulivu kabisa huku mvua ikiwa inapigapiga katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam, direct tutakwenda kuangalia app ambazo ni hatari kukaa kwenye simu yako na ikiwezekana ungezifuta kabisa.

Najua unabashasha na unataka kuzifahamu ni app zipi hizo? Twende sawa na dondoo ya leo haikuachi patupu!!

App zenye kutaka ruhusa nyingi

Ni dhahiri kuwa ili app yeyote iweze kufanya kazi kwenye simu yako inahitaji ruhusa nyingi kupitia uwezo wa app, kuna wakati unataka kufungua game kwenye simu yako na inahitaji ruhusa kama vile uwezo wa kuona namba ya simu, mahali ulipo (location) na mengine mengi.

Suala kama la kuangalia game halina haja eti lazima upate ruhusa ya kuona namba zako za simu, mbali na game pia zipo app nyingi ambazo zinahitaji ruhusa ambazo sio za lazima kwenye app husika.

Ukiwa unatumia simu yenye mfumo mpya wa android 11 na ni muhimu kwa wewe kuruhusu app fulani kutumia permission Fulani, basi tumia sehemu ya allow only once.

App za kuongeza RAM

Awali mfumo wa android ulipokua unaanza kutumika ni wazi kuwa apps za kuongeza uwezo wa RAM zilikua maarufu sana, lakini kwa miaka ya hivi karibuni mfumo wa android sasa umeboreshwa na hakuna simu yoyote ambayo inazinduliwa yenye uhitaji wa kuongeza app ya RAM hivyo hakuna haja ya kuwa na app kama hizi kwenye simu yako.

Kwa mujibu wa Beeboom baadhi ya app hizi huchukua data zako muhimu kutoka kwenye file mbalimbali ambazo inadai inazifuta hivyo kama unatumia simu ya kisasa huna haja kabisa na app hizi zinazodai kuongeza uwezo wa RAM kwani simu nyingi za sasa zinakuja na sehemu ya kufuta apps zinazochukua nafasi kubwa kwenye simu yako.

Ndiyooo!!!, hizo ni baadhi tu ambazo nimekuandalia kwa leo katika kipengele cha Smartphone be careful and make sure unaipambania simu yakoooo!!.

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post