Karim Pembe kijana aliyejifunza kazi ya Graphics kupitia Youtube

Karim Pembe Kijana Aliyejifunza Kazi Ya Graphics Kupitia Youtube

Wajuzi wa mambo wanasema ukitaka kufanikiwa ama kupiga hatua kwenye maisha yako basi hakikisha unaambatana na mambo matatu muhimu ambayo ni nidhamu, ubunifu pamoja na kujituma.

Je unayafahamu hayo kijana mwenzangu? Its Monday bhana tunakutana tena kwenye zile makala za kazi, ujuzi na maarifa ambapo leo nakukutanisha naye kijana mdogo sana anayetambulika kwa jina la Karim Pembe.

Karim Pembe  maarufu kama Kp graphics ni kijana mbunifu anayejihusisha na kazi ya Graphics Disagner akiwa na misingi mikuu miwili inayomsaidia zaidi katika kufanya vizuri kwenye kazi zake.

Kwa mujibu wa Pembe Kazi ya graphics ni kazi ambayo inahusisha zaidi usanifu wa matangazo ambapo imegawanyika katika sehemu mbili ikiwemo online graphics na printing graphics.

Akizungumza na jarida la kijanja la vijana la Mwananchi Scoop ambalo lengo na dhamira ya magazine hii ni kuibua ujuzi, vipaji pamoja na maarifa mbalimbali ambayo vijana wanayafanya katika maisha yao ya kila siku.

Pembe alisema kuwa  kupitia mtandao wa Youtube ameweza kujifunza zaidi kazi hiyo ambayo  imemsaidi sana kupiga hatua kwa kuzingatia misingi yake ambayo amejiwekea ikiwemo suala zima la nidhamu, usikivu na kujituma.

Aidha alisema mitandao inakila kitu kwani kupitia internet mtu anaweza kujifunza kitu chochote ambacho anataka kufanya pasipo na vikwazo.

Vilevile alisema alivutiwa sana na kazi hiyo kutokana na rafiki yake ambaye alikuwa akiifanya hivyo aliamua kupambana na kujifunza kupitia mtandaoni.

Pia alisema ili vijana waweze kufanya vizuri zaidi kwenye shughuli zao wahakikishe wanazingatia misingi ya kazi zao.

Hata hivyo alisema kazi hiyo ikotofauti sana na fani nyingine kwani haihitaji kusomea ili uweze kuwa disagner mzuri bali inahitaji sana passionate, kujibidiisha na   kufanya mazoezi kila siku.

Pia alisema kazi hiyo inahitaji sana muda kwani wapo watu ambao wamesomea lakini hawafanyi vizuri kutokana na kutokuipenda na kutokuifanyia mazoezi hivyo mtu asipofanya mazoezi basi kuwa graphics mzuri ni ndoto.

“Kitu usichokipenda inakuwa marachache sana kufanya mazoezi na usipofanya mazoezi basi kazi itakua ngumu sana kwako lakini unaweza kujifunza pia graphics online kupitia youtube”alisema.

Aidha kijana huyo alisema kitu ambacho anajivunia kwenye kazi yake ni suala la kukuza Brand za biashara za watu jambo ambalo linamfanya aone ukubwa wa kazi anayoifanya.

“Najivunia kukuza brand za watu kama unavyojua biashara ni matangazo na kupitia matangazo ambayo nawadizainia watu yamewasaidia kukuza biashara zao”alisema.

Hata hivyo alisema kutokana na kazi hiyo imemsaidia pia kukutana na watu mbalimbali na kujiingizia kipato kama kijana kwani anakidhi mahitaji yake muhimu.

Sambamba na hayo amezungumzia utofauti wa kazi yake na magraphics disagner wengine ambapo alisema creativity ndio inayomsaidia zaidi.

“Mimi najitahidi kila ninapofanya kazi basi nahakikisha nafanya zaidi ya kile alichokitarajia hivyo najitahidi kubuni kitu kipya kiasi kwamba mteja akiona anakubali na kusema woow”alisema.

Kama tunavyofahamu penye nia pana njia basi kila jambo lina ugumu wake na changamoto zake kijana pembe alifunguka kuhusiana na changamoto ambazo anakabialiana nazo ikiwemo watu kutaka kufanyiwa kazi zao bila malipo.

Aidha alisema wakati mwingine changamoto anayokutana nayo ni pale anapomtajia mteja bei ya kazi ambayo amempatia hivyo huleta sintofahamu baina yake na mteja.

Hata hivyo alisema anamalengo ambayo amejiwekea kupitia kazi anayoifanya ikiwemo matarajio yake makubwa ni kuhakikisha anakuja kumiliki visual house yak wake binafsi.

“Kiukweli matamanio yangu siku moja niweze kuwa na visual house ambayo tutakuwa tunatengeneza vitu vyenye ubora zaidi vitakavyo shindanishwa na wenzetu wanchi mbalimbali”alisema

Hata hivyo alisema akifanikiwa kupiga hatua hiyo itakuwa rahisi kuweza kuwashika mkono vijana wengine ambao wana ndoto na malengo ya kufanya kazi za ubunifu.

Sambamba na hayo alitoa ushauri kwa vijana ambao wanachipukia kwenye fani ya graphics akiwataka wazidi kujifunza zaidi na wasibweteke kwani kadri wanavyozidi kujifunza ndivyo wanavyokuwa bora zaidi.

Vilevile alisema nidhamu ndiyo kila kitu kwani bila ya nidhamu huwezi kufanya kitu chochote hivyo kazi yoyoyte ile inahitaji nidhamu ya hali ya juu ili uweze kufanya vizuri zaidi.

“Kwenye nidhamu unapata kila kitu, utapewa kazi ya mtu bila ya kuiheshimu utafanya kawaida hivyo tutambue kuwa mteja unayempata mwanzo ndiyo atakayekuletea mteja mwingine”alisema.

Nikukumbushe kuwa kijana Pembe amemaliza elimu yake ya Chuo kikuu katika chuo cha Institute of Financial Management (IFM )miezi michache iliyopita akiwa amechukua course ya  bachelor of insurance and Management.

Vilevile kijana huyo imedhihirika kuwa graphics sio course aliyosemea chuoni lakini kupitia elimu, ujuzi na maarifa mbalimbali ambayo aliyatumia katika kujifunza ndiyo yaliyonmsaidia kufanya kazi yake hiyo.

Mfahamu kwa ufupi.

Karimu Pembe alifanikiwa kupata elimu ya msingi katika shule ya Mwanayamala na kujiunga sekondari shule ya kitunda na hatimaye Advance akafanikiwa kumaliza Makongo high school.

 

 

      
Comments 3


 • Awesome Image
  Shani Amiri

  Uthubutu na kujituma, nidham ndo msingi wa mafanikio big up kareem pambana uzifikie ndoto zako nyingine naimani na wengine waitaiga kutoka kwako Allah azidi kukusimamia

 • Awesome Image
  Member

  Never stop learning because Life never Stop Teaching also More blessings #Kazi IENDELEEE

 • Awesome Image
  Member

  Never stop learning because Life never Stop Teaching also More blessings #Kazi IENDELEEE

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.

Latest Post