Karen: Endeleeni kumuombea baba angu

Karen: Endeleeni kumuombea baba angu

Mwanamuziki #MalkiaKaren amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwenye msiba wa Baba yake mzazi  aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM,  Gardiner Habash.

Kupitia #Instastory yake Karen ameandika:

 "Kipekee nitoe shukran za dhati sana kwenu nyote kwa salamu za pole na za faraja Mwenyezi Mungu akawe nanyi. Tuendelee Kumuweka kwenye Maombi Mpendwa wetu Apumzike kwa Amani."

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mtangazaji huyo alipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags