Kapombe Atunukiwa tuzo mchezaji bora

Kapombe Atunukiwa tuzo mchezaji bora

Ooo h yes!! Beki wa klabu ya Simba SC Shomari Kapombe, amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Februari wa mashabiki wa klabu hiyo (Fans Player of the Month), ameshinda kiasi cha shilingi milioni 2 .

Kapombe ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku wachezaji wenzake aliokuwa akishindana nao kuwania tuzo hiyo ambao ni winga Peter Banda na mlinzi wa kati Henock Inonga ambao aliingia nao fainali katika kinyang’anyiro hicho. Katika mwezi Februari Kapombe alicheza mechi 4 ambapo alifunga bao 1 na alihusika kwenye kutengeneza mabao mengine 2.

Baada ya kushinda tuzo hiyo beki huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars amesema tuzo hiyo ni muhimu kwao kama wachezaji kwasbabau inawaongezea hali yakupambana zaidi,

“Kwanza niwashukuru Emirate kwa kudhamini tuzo hii, inaongeza morali kwetu kama wachezaji. Pia niwashukuru wachezaji wenzangu kwa ushiriakiano mkubwa walionipa. Kwangu hii ni changamoto ambayo inanifanya niendelee kujituma kwa ajili ya kuisaidia timu kufanya vizuri na ndio lengo la kila mchezaji wa Simba.” amesema Kapombe.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags