Baada ya Rais wa Marekani Donald Trump na mkali wa Pop Taylor Swift kutangazwa kuwepo katika fainali za ‘Super Bowl LIX’, sasa inaelezwa kuwa rapa Kanye West na mkewe Bianca huwenda wakawepo katika mchezo huo.
Mapema wiki hii mapaparazi walimnasa Ye katika mitaa ya Los Angeles na kumuuliza kama mipango yake ya kuhudhiria kwenye fainali hizo ndipo akajibu kuwa yeye na mkewe, Bianca Censori, huenda wakawepo New Orleans kushuhudia mchezo huo.
Ikumbukwe kuwa Kanye na Swift hawapiki chungu kimoja hivyo huwenda msanii huyo asihudhurie kabisa katika mchezo huo kwani miaka ya nyuma Swift alimfanya Kanye aondolewe uwanjani baada ya kununua tiketi ya Ye kwa pesa ya juu zaidi.
Aidha kufuatia taarifa hiyo baadhi ya mashabiki wamekuwa wakionesha kutokubaliana na wawili hao kuhudhuria katika tamasha hilo kuhofia mavazi yao, baada ya kile kilichotokea katika usiku wa tuzo za Grammy ambapo Censori alivalia gauni linalimuonesha mwili mzima.
Fainali za Super Bowl LIX inatarajiwa kufanyika Jumapili Februari 9, 2025 katika uwanja wa Caesars Superdome huko New Orleans huku Kendrick Lamar akitumbuiza wakati wa mapumziko katika mchezo huo.
Leave a Reply