Kanye West hashikiki Spotify

Kanye West hashikiki Spotify

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu kuachiwa kwa albumu ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Kanye West, ya ‘Vultures 1’ ambayo ameshirikiana na ‘rapa’ Ty Dolla Sign, albumu hiyo imeendelea kufanya makubwa katika kipindi kifupi kupitia mtandao wa Spotify baada ya ngoma yake ya ‘Back to Me’ kufikisha streams milioni 50.

Hii inakuwa nyimbo ya nne kutoka kwenye albumu hiyo ya Kanye, lakini pia inakuwa ni nyimbo yake ya 179 kufikia hatua hiyo.

‘Vultures 1’ iliachiwa Februari 10 mwaka huu ambapo imefanikiwa kuuza zaidi ya nakala 148,000 nchini Marekani, huku Kanye kutokana na mafanikio hayo yupo mbioni kutoa ‘Vultures 2’ ambayo kwa mujibu wa vyombo vya habari Marekani huenda ikatolewa mwezi Machi au Aprili mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags