Kanye West atangaza kustaafu muziki

Kanye West atangaza kustaafu muziki

Mwanamuziki wa hip-hop kutoka nchini Marekani, Kanye West ametangaza kustaafu muziki huku akidai kuwa hana uhakika wa kufanya kitu kingine kinachohusiana na muziki.

Kanye mwenye umri wa miaka 47 alizungumza hayo kupitia kipindi maalum cha Rich The Kid Jumanne Julai 9, akidai kuwa ana staafu muziki

“Nastaafu muziki kitaaluma ingawa sina uhakika nini cha kufanya hapo baadaye” alisema.

Hata hivyo kupitia kipindi hicho mashabiki na watazamaji walionesha kushangazwa na kauli ya Kanye huku wakida kuwa bado mwanamuziki huyo anahitajika katika gemu kwa kiasi kikubwa.

Utakumbuka kuwa Kanye West ni mmoja wa watu mashuhuri katika hip-hop ulimwenguni, alianza kazi yake ya muziki miaka ya 2000 kama mtayarishaji huko Chicago baada ya kuacha chuo kikuu.

Mwaka 2001 alipata umaarufu baada ya kutayarisha albamu ya Jay-Z ‘The Blueprint’ na baadaye akatiwa saini kama mtayarishaji wa ndani wa Roc-A-Fella Records.

Mwaka 2004, West alitoa albamu yake ya kwanza, 'The College Dropout,' ambayo ilipokelewa kwa sifa kubwa na akatoa wimbo wa 'Slow Jamz, uliowahi kushika namba moja ‘Billboard Hot 100’ nchini humo.

Pia ni msanii wa Hip-hop aliyepewa tuzo nyingi zaidi katika historia ya Tuzo za Grammys pamoja na Jay-Z wenye ‘Golden Gramophones’ 24 mapaka sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags