Kanye na mpango wa kufanya ziara ya dunia

Kanye na mpango wa kufanya ziara ya dunia

Mwanamuziki na mwanamitindo kutoka nchini Marekani Kanye West anaripotiwa kuwa na mipango ya kufanya ziara ya dunia miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa tovuti ya #Billboard, Kanye atafanya kazi na aliyekuwa meneja wake John Monopoly kwa ajili ya kuandaa ratiba na mipango mizima ya ziara hiyo ambayo huenda ikifanyika majira ya joto.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Kanye kufanya ziara ni mwaka 2016, ikiwa ni ziara yake ya tano iliyopewa jina la ‘Saint Pablo Tour’ lakini haikukamilika kutokana na #Kanye kupata matatizo ya kiafya na kupelekea kulazwa hospital.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags