Kanye na Drake warudisha bifu lao

Kanye na Drake warudisha bifu lao

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu wanamuziki kutoka nchini Marekani #KanyeWest na #Drake wamerudisha tena bifu lao baada ya Kanye kudai kuwa ‘rapa’ huyo amekabidhi nafsi yake kwa shetani ndiyo maana anamsema.

Kanye ameyasema hayo kupitia Podcast ya ‘The Download’ amedai kuwa Drake ameenda kinyume na Mungu anavyotaka kwa kukabidhi nafsi yake kwa shetani ili agombane na yeye.

Inadaiwa kuwa bifu la wawili hao linatokana na ushindani wao katika muziki huku kila mmoja akitaka kuonekana bora kuliko mwenzie ambapo hivi karibu Kanye ameachia wimbo uiitwao ‘Like That’ aliyomshirikisha #Metroboomin ukidaiwa kuwa ni dongo kwenda kwa Drake.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2021 wawili hao walikuwa kwenye bifu kama hilo, lakini Desemba mwaka huo huo walimaliza bifu lao na kufanya tamasha la pamoja nchini humo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags