Kanye ataka watu wamuite Ye

Kanye ataka watu wamuite Ye

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Kanye West, inaonekana amechoshwa na watu kutumia jina lake la zamani la Kanye na badala yake kuwataka watumie jina jipya la kisheria.

Kufuatiwa na mahojiano yake aliyoyafanya na mtangazaji wa runinga ya Revolt Justin Laboy, siku ya jana Februari 28, 2024, ameeleza kuwa ataifunga akaunti yake ya Instagram inayotambulika kwa jina la Kanye West na kufungua mpya kwa jina lake la kisheria la Ye.

Hata hivyo hapo awali ilikuwa ni ngumu kwa Kanye kupata ukurasa wenye jina la YE kwani yupo anayetumia jina hilo, lakini baada ya muda mfupi mtandao wa Instagram uliridhia mwanamuziki huyo kupewa akaunti itakayokuwa na jina la YE.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2021, jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la kubadili jina la kisheria la YE. Kanye alifanya uamuzi huo kutokana na albamu yake ya nane kubeba jina hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags