Kanye ajitetea kuhusu Wayahudi

Kanye ajitetea kuhusu Wayahudi

Mwanamuziki Kanye West amefunguka kuwa wakati anatoa kauli za chuki dhidi ya Wayahudi alikuwa amelewa.

Kanye ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na mwanadada Candace Owens akidai kuwa wakati anatoa maneno yale ya chuki hakua yeye bali zilikuwa ni pombe.

“Wakati natoa maneno yale ya chuki nilikuwa nimelewa, unataka kujua nilikunywa pombe gani ambayo nilikuwa nayo ndani ni Hennessy, na hapo ndiyo niliamini kuwa kinywaji hicho kinaweza kukutoa kwenye utulivu kabisa”

Hata hivyo aliongezea kwa kudai kuwa baada ya pombe kuisha hakuweza kutengua kauli yake kutokana na hakutaka maneno yake yadharauliwe licha ya kuwa yanakera sana kwani baadha ya maneno aliyoyaongea yalikuwa ni sahihi kabisa.

Utakumbuka kuwa mwaka 2022 Kanye alitoa kauli za chuki kwa Wayahudi zilizopelekea kupoteza mikataba ya kazi na kampuni mbalimbali ikiwemo Gap na Adidas .

Hii siyo mara ya kwanza kwa Kanye kujitetea kupitia pombe kwani mwaka 2009 aliwahi kukatiza hotuba ya Taylor Swift kwenye VMAs na kuanza kutoa maneno machafu, ambapo baadaye alijitetea kuwa siku hiyo alikunywa Hennessy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags