Kanjanja mkware nikatia timu msibani…!

Kanjanja mkware nikatia timu msibani…!

Nakumbuka ilikuwa ni mwishoni mwa miaka ya 1990, ndipo tukio hili liponitokea.

 

Baada ya kupata misukosuko kadhaa hapa jijini Dar, kutokana na mbilinge zangu za ujanani kuwania vimwana, nilipata wazo la kubadilisha upepo na kwenda kwa mjomba wangu aliyekuwa akifanya kazi mkoani Tabora.

 

Mjomba alikuwa akiishi eneo moja liitwalo Cheyo, aneo ambalo ni maarufu sana mkoani Tabora kwa sababu wanaoishi eneo hilo ni watu wenye nafasi kidogo, yaani ni kama vile unazungumzia Masaki au Oysterbay kwa hapa Dar.

 

Mjomba alikuwa anaishi na mkewe na watoto wake wawili wa kiume ambao bado walikuwa bado wadogo, wa kwanza akiwa na miaka mitano na wa pili akiwa na miaka mitatu.

 

Nilipofika mjomba aliniahidi kunifanyia mipango ya kwenda kusoma chuo cha ualimu, lakini kwa kuwa nilikuwa nimechelewa ilinipasa nisubiri hadi mwakani. Hata hivyo nilipata wazo.

 

Kwa kuwa mjomba alikuwa na kamera yake aina ya Yashica aliyoinunua nchini Japani alipokwenda kwa mafunzo mafupi, nilimuomba niitumie kwa kupiga picha za mitaani na kujipatia kipato.

 

Mjomba alinikubalia na nikaanza kazi hiyo mara moja kwa kurandaranda mitaani na baiskeli yake na hiyo Kamera nikipiga picha.

 

Haikuchukua muda nilianza kuwa maarufu pale katika viunga vya cheyo na maeneo ya jirani kwa sababu nilikuwa natoa picha nzuri sana.

 

Umaarufu huo ulinipelekea nianze kubabaikiwa na vidosho, maana ile kujulikana kwamba natokea Dar kulinipa credit ya kuwabadilisha mabinti nitakavyo.

 

Haikuchukua muda tabia yangu hiyo ya kuchukua vibinti vya shule ikaniletea kisirani ikiwa imebaki mwezi mmoja kujiunga na chuo cha ualimu.

 

Nakumbuka mjomba aliniita na kuniambia kwamba amepata fununu kuwa kuna binti mmoja ambaye baba yake anafanya kazi usalama wa taifa nimempa ujauzito, na hivyo natafutwa na Polisi, aliniambia kwamba muda wowote nitakuja kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kumpa mwanafunzi Mimba.

 

Taarifa zile hazikuwa nzuri kwangu kwani nilibabaika sana, lakini nilijikaza kiume nisionyeshe hisia hizo za kubabaika kwa mjomba.

 

Nilisimama kidete kukanusha taarifa hizo, lakini mjomba aliniambia kwamba nitakapofikishwa mahakamani ndio ukweli utajulikana, kisha akaondoka kwenda kazini.

 

Huku nyuma shangazi alinishauri nitoroke maana huyo baba wa binti ni mtu wa Musoma, anaweza kunifanyia kitu mbaya.

Ni kweli nilitorokea kwa rafiki yangu na kujificha na siku iliyofuata nilipanda Treni na kurudi Dar na kuepuka kifungo cha kumtia mimba binti wa shule.

 

Nilipokuwa Dar niliendea na kazi yangu ya kupiga picha baada ya kununua kamera kutokanana fedha nilizojikusanyia nilipokuwa Tabora. Siku zilienda, nikasahau kuhusu tukio hilo na maisha yakaendelea.

 

Katika pilika pilika zangu hizo za kupiga picha, nilipata wazo la kutafuta kitambulisho cha uandishi wa habari ili niweze kujipenyeza kwenye mahoteli makubwa na kupiga picha za matukio mbalimbali ili kujiongezea kipato, wazo hilo nililipata kutoka kwa rafiki yangu mmoja ambaye yeye alikuwa ni mwandishi wa habari na mpiga picha by professional. Alikuwa anatengeza fedha kweli kweli kwa kuhudhuria semina mbalimbali na kujipatia posho achilia mbali kuuza picha.

 

Ni kweli nilifanikiwa kupata hicho kitambulisho na sasa nikawa najulikana kama mwandishi wa habari, ingawa sikuwa mwandishi wa habari bali  mwandishi wa habari feki ambapo hujulikana kwa jina maarufu la Kanjanja.

Ilitokea siku moja ulitokea msiba wa mke wa mzee mmoja ambaye alikuwa ni bosi mkubwa kabisa katika wizara fulani.

 

Msiba huo ulivuta watu wengi kutokana na umaarufu wa mzee huyo kiasi cha kutembelewa na viongozi mbalimbali wa serikali. Yule rafiki yangu aliitwa kwa ajili ya kupiga picha, hivyo akaniomba nifuatane naye, ili tuwe wawili.

 

Tulifika pale msibani majira ya mchana na kuanza kupiga picha kila wageni wanapofika hapo msibani ikiwa ni pamoja na matukio mengine madogo madogo.

 

Nikiwa katika pilika pilika zangu za kupiga picha, nikaitwa na kijana mmoja, nakunieleza kuwa ninaitwa na mzee mmoja aliyekuwa amesimama na binti mmoja.

 

Nilipofika pale nilidhani wanataka kupiga picha, lakini yule mzee aliniambia kwamba hakuniita ili kupigwa picha bali kulikuwa na jambo anataka kuniuliza. Yule binti ambaye awali sikumjua kutokana na kujitanda ushungi alikuwa akiniangalia kwa jicho kali mpaka nikaogopa.

 

“Samahanin kijana, eti unamjua huyu binti…” yule mzee aliniuliza.

“Hapana mzee simfahamu kabisa…….” 

 

Nilimjibu yule mzee lakini yule binti alinikata kalma,

“Ina maana leo unajifanya hunijui wewe…….., (alitaja jina langu) wakati uliponipa mimba kule Tabora na kuniharibia masomo na kisha kutorokea Dar ulidhani hatutakutana..? 

 

Alisema yule binti wa Kijita huku akiwa amefura kwa hasira na kisha akamgeukia yule mzee na kumwambia, “Mjomba ndiye huyu huyu, na wala si mwingine……….”

 

Nilibabaika kidogo.

Ni kweli, nilipomtazama vizuri yule binti nilimkumbuka sasa, kwani alikuwa amebadilika sana na alikuwa mzuri kweli kweli kutokana na kuoga maji ya Chumvi ya Dar….

 

“Kijana, huyu binti hana sababu ya kukusingizia, kuwa mkweli tuyamalize haya mambo la sivyo utaozea jela, usicheze na serikali kijana….” Yule mzee aliongea kwa ukali kidogo huku akiwa amenikazi macho…

 

Nikajua sasa mambo yameshaharibika, lakini sikukubali, nilikanusha vikali na kusisitiza kwamba wamenifananisha.

“Naona wewe hutaki suluhu, sasa itabidi tukazungumzie Oystabay Polisi.” Alisema yule mzee huku akitoa simu yake ya mkononi ili kupiga simu polisi.

 

Niliposikia habari ya Oystebay Polisi, nilikurupuka na kutimua mbio zisizo za kawaida, yule mzee aliwaita vijana wake  na kuwa amrisha wanikamate lakini wapi, niliwaacha mbali sana, nikawa nime save kutoka kwenye kadhia hiyo.

 

Baadae nilitafuta wazee na kwenda kuzungumza na yule mzee mbaye alikuwa ni mjomba wa yule binti na kuyamaliza ambapo pia nilipata bahati ya kumuona mwanangu wa kiume. Alikuwa na miaka mitano wakati huo.

 

Nilikuja kugundua kwamba yule binti alijifungua salama kisha akaja Dar kwa mjomba wake na kuendelea na masomo ambapo kipindi hicho alikuwa yuko chuo kikuu akiso


Comments 3


 • Awesome Image
  Flora nnko

  MUNGU azid kukuinua zaid na zaid tuendleee kufurahia mafundsho yako yanatufarj sana yanatuvusha sehem 1 kwenda nyingne

 • Awesome Image
  Hope efeso

  Kwakweli najivunia na kujiona ni mtu mwenye bahati sanaa kufahamiana na wewee kakaangu, jamani hongera mnoo nakuombea heri siku zote uzid kuwa imara kakaangu naimani .Mungu atakuonyesha njia pasipo na njia

 • Awesome Image
  RUTH JULIUS MBWILO

  Nakukubalii Sana yaani unanifanya nijifaliji kupitia clip zako autoishia hapa utafika mbele zaidi Tena mnook god blec ur job I pray for japo sijawahi kukutia machoni ila mungu akupe muangaza ufike mbali zaidi ya hapa dunia kiujumla ikujue mnoooo kwani unakosha watu walopata pain ya mapenzi like me nilitamani hata kulewa kufanya vitu vya ajabu ila nkiangalia clip zako najiona kumbe sifai kufika wapo waloumizwa kunizid❤️❤️❤️

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Mzee Mtambuzi

A freelance Journalist and also teaching self-empowerment, positive thinking as a means of creating the life you desire including spirituality. He is writing in Mwananchi Scoop every Wednesday Visa na Mikasa.


Latest Post