Kamari yamponza Tonali

Kamari yamponza Tonali

Mchezaji wa ‘klabu’ #NewcastleUnited, #SandroTonali amefungiwa miezi 10 kujihusisha na masuala ya ‘soka’ kwa kukiuka sheria za michezo ya kubashiri (kamari) nchini #Italia.

#Tonali mwenye umri wa miaka 23 atakosa msimu mzima wa ‘klabu’ yake ya Newcastle United sambamba na michuano ya #EURO2024 na ‘timu’ ya Taifa Italia.

Tonali alijiunga na ‘timu’ hiyo Julai mwaka huu akitokea ‘klabu’ ya #ACMilan amekiri kubashiri ‘mechi’ za ‘timu’ yake ya zamani wakati akiwa ‘klabuni’ hapo jambo ambalo ni kinyume na sheria za #Italia.

Wanasoka wa kulipwa nchini #Italia hawaruhusiwi kucheza kamari kwenye mashindano yoyote yanayoandaliwa na #FIFA, #UEFA au #FIGC huku adhabu ikiwa ni kifungo cha miaka mitatu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags