Kama tendo umelikinai, fanya hivi!

Kama tendo umelikinai, fanya hivi!

Kwa mwanamke kukinaiwa na tendo si kitu cha kustaajabisha. Kwa wanawake tendo kwao sio kama wanaume kuingiza na kumaliza basi.

Kwa wanawake tendo linaenda sambamba na maandalizi kihisia linahitaji utulivu wa moyo na akili huku ikichagizwa na upendo kwa mwenzi wake tofauti na wanaume ambao kwao hamu ya tendo ipo kwenye uume, ukisimama tu adandie.

Inaweza kutokea mwanamke akaishiwa na hamu ya tendo la ndoa kwa mwenzi wake si kwa sababu hampendi bali ni kutokana na tendo hilo kukosa ubunifu na kufanyika kwa namna hiyo hiyo mahali pale pale mandhari ile ile kila siku, kwa mwanaume siyo issue lakini kwa mwanamke jambo hilo lina mchango mkubwa katika kusababisha mwanamke kukosa hamu ya tendo na kujikuta anajifanyia tu

Hapa chini ninaeleza machache kuhusu namna ya kuboresha hamu ya tendo kwa wapenzi nakuondoa hali ya sintofahamu kwa wapendanao:

  1. Tengeneza mazingira ya chap chap: Kufanya tendo la mshitukizo.

Hapa ningependa kutumia neno chap chap lina utamu wake jamani kama hujawahi kujaribu nawashauri mjaribu. Tendo la ndoa la kustukiza linawehusha hasa panapotokea hakuna maandalizi yoyote rasmi mnajikuta mko mahali na mazingira yanaruhusu na mnajikuta wote mnapatwa na hamu ya hali yajuu ya kukutana kimwili mnajikuta mkikabiliana huku mihemko yenu ya kufanya tendo ikiwa imewapanda huo utamu wake hausimuliki.

Tendo la kushtukiza linatakiwa litengenezewe na mazingira na mwanamke kwa kufanya uchokozi kwa mwenzi wake kwa kumtumia meseji za kushawishi zenye kutia hamu ya kujamiiana na kuwa na ubunifu wa kuandaa mazingira kuwa rafiki ya kumvutia mwenzi wake katika kuamsha hamu ya kukutana kimwili, yaani mwanaume akikutana na mpenzi wake damu inaanza kumchemka kutokana na kushawishiwa kivitendo au lugha ya mwili.

  1. Kiwanja ni muhimu:

Kuchagua kiwanja cha kukutaniana mwenzi wako tofauti na mazingira uliyoyazoea husaidia sana kuamsha matamanio ya tendo la ndoa kwa wapendanao kuliko inavyofikiriwa.

Katika kuchagua kiwanja haitakiwi iwe ni maalum sana (too special) kivile, inaweza kuwa ni eneo la wazi mbali lakini lisiwe ni eneo linalokutanisha watu kwani inaweza kuwa karaha badala ya kujipa raha, kwa mfano mnaweza kwenda South Beach Kigamboni kwa wakazi wa Dar mkatafuta eneo tulivu mkapaki gari lenu na kama eneo lina ukimya wa kutosha na hakuna watu wanaopitapita hapo mkamaliza mambo yenu humohumo kwenye gari huku mkijiachia kwa raha zenu

Au kwa Zanzibar beach kama ya Kizimkazi inaweza kuwa mahali pazuri, lakini pia kuna hoteli zilizoko pembezoni mwa bahari ya Hindi au Mbuga za wanyama ambazo kwa wenye uwezo wanaweza kuzitumia vyema kufanikisha jambo hilo au hoteli yoyote iliyoko nje ya mji yenye utulivu na gharama zake ni nafuu.

  1. Kilainishini muhimu:

Ingawa wanawake wana kilainishi cha kimaumbile katika maumbile yao ya uke (naturally lubrication), lakini wakati mwingine maumbile yanaweza kuchelewesha kilainishi wakati wa tendo la kushtukiza, hapa naomba ieleweke kwamba kuna wakati tendo la kushtukiza linaweza lisiwe na maandalizi makubwa sana kutokana na kila mmoja kuhemkwa na hiyo haisababishi maumbile ya uke kutoa ushirikiano haraka kama inavyotarajiwa.

Kuna wanawake wengine maumbile yao yanajivuta katika kutoa kilainishi na ndiyo sababu inashauriwa kuwa na kilainishi cha ziada ambacho kinapatikana kwenye maduka ya dawa maarufu kama KY naamini wengi wanajua kilainishi hiki ambacho kinazalishwa na kampuni ya Johnson Johnson.

Kilainishi hiki kinatakiwa kiwekwe katika eneo ambalo kitapatikana kiurahisi kwa sababu kikiwekwa mbali na mkiwa mmehemkwa halafu mmoja akaondoka kwenda kutafuta ukapita muda anahangaika kutafuta basi hapo tena mizuka itakuwa imeshuka na kutakuwa hakuna kile kinachoitwa cha chap chap

  1. Mavazi ya uchokokozi yanayochojoka haraka muhimu:

Jamani Kama mwanamke anataka kufanya maandalizi ya kile kinachoitwa cha chap chap aina ya mavazi anayotakiwa kuvaa ni kitu muhimu kuzingatia, siyo mtu unatarajia mpenzi wako akija mpige cha chap chap halafu umekomelea msuruali wa jinzi ulioushika mwili.

Mwanamke anatakiwa ahakikishe anavaa nguo nyepesi zinazoyachora maungo yake na zenye kumpa mwanaume ushirikiano akitaka kuzivua wakati wa zoezi hilo la chap chap.Kwa jinsi mwanaume atakavyopata urahisi kusasambua nguo za mpenzi wake ndivyo ambavyo mwanamke atalifurahia tendo.

Ngojeni niwamegee siri, kasketi kafupi bila nguo ya ndani au kijigauni chepesi kinaweza kutoa ushirikiano mzuri tu kwa mwanaume

  1. Angalia aina ya mkao utakaokupa uhuru wa kujiachia utakavyo:

Zingatia mkao wowote utakaokupa nafasi au uhuru wa kujiachia utakavyo wakati wa tendo la chap chap ili uweze kulifurahia tendo wewe na mwenzi wako.

Mkao ambao utakuletea maumivu wakati wa tendo utakatisha hamu yote na kujikuta tendo hilo likiwa karaha kwako na siyo kukupa raha

  1. Usijisikie aibu kujiachia:

Wote tunajua kwamba tendo la kujamiiana ni la kimaumbile kwa hiyo kulifanya nikujikamilisha.

Hivyo si vyema kulionea aibu, jiachie mwanamke utakavyo, piga mabusu tembeza ulimi kwa mwenzi wako kama chatu anavyoandaa kitoweo chake na mkono wako ufanye kazi ya ziada kumpapasa mwenzi wako kila kona ya mwili wake. Hakikisha mnapeana ushirikiano ili wote mfike kileleni kwa pamoja.

 

Niambie mshkaji wangu, wewe ukikinai unafanyaga nini?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post

Latest Tags