Kajala Masanja avutiwa na Serena Williams

Kajala Masanja avutiwa na Serena Williams

Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja amesema anafanya mazoezi kila siku kwa sababu anatamani kuwa kama mcheza Tenisi maarufu duniani, Serena Williams.

Serena ambaye ni ndugu na Venus Williams, wamewahi kutamba kwenye mchezo huo kwa miaka mingi na kushinda mataji makubwa ya dunia likiwamo maarufu la US Upen na lile la Wembledon na kwa sasa wanaendelea na mazoezi kama ilivyo kwa Kajala ili kuendelea kuwa fiti.

Kajala amesema mazoezi ni kitu ambacho kipo kwenye damu yake na anapendelea sana kwenda kufanya asubuhi maana akimaliza anafanya mambo yake jioni kama siku za wikiendi.

Amesema tangu aanze sasa ni miaka minane na anafanya ili kujiweka fiti ingawa pia kuna ishu ya daktari aliyemshauri, ingawa wengi wanajua anafanya kwa sababu anatafuta shepu kama wengi wanavyofanya.

Kwa kuzungumzia shepu yake, amesema anashukuru Mungu kwani tayari anayo na si ya kutengeneza bali amemjaliwa.

"Mazoezi ni kitu ambacho kipo kwenye damu yangu. Napendelea sana kwenda kufanya asubuhi maana nikimaliza nafanya mambo yangu jioni hasa siku za wikiendi. Pia natamani sana kuwa kama Serena Williams kwa ufanyaji wake wa mazoezi na sio nafanya kwa ajili ya kutengeza shepu kama baadhi ya watu wanavyodhani wakati shepu ni asili yangu."

"Kwa sasa nina miaka minne tangu nimeanza kufanya mazoezi, lakini nishajenga mazoea na nisipofanya najiona kama mgonjwa hivi," amesema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags