Kajala atangaza kuwa single

Kajala atangaza kuwa single

Moja ya story zinazobamba huko mitandaoni ya msanii wa filamu Kajala Masanja ambaye amefunguka na kusema kuwa anabaki kuwa single.

Itakumbukwa kuwa Kajala alishawahi kuwa katika mahusiano na mwanamuziki Harmonize lakini uhusiano wao haukudumu na hivyo waliachana huku wakirushiana maneno makali na tuhuma nzito.

Basi kutoka kwenye ukurasa wa Instagram yake Kajala aliandika ujumbe uliyokuwa ukisomeka “Nina hitaji kukaa peke yangu, kwa sababu nikimpenda mtu napenda kupita kiasi, ni ngumu sana katika kizazi hiki sababu penzi hilo halithaminiwi tena,” aliandika.

Tuambie mpenzi msomaji wetu unadhani uwamuzi wa Kajala ni sahihi kwake au anatuzuga tu, dondosha comment yako katika ukurasa wetu wa Instagram pale.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post