Kajala amjibu kimafumbo Harmonize

Kajala amjibu kimafumbo Harmonize

Ohoo Msanii wa filamu nchini  Kajala Frida ameshea ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram kupitia  'Insta Story' ambao unasemekana ni muendelezo wa majibu kwa Harmonize ambaye anaonesha wazi kutaka kurudiana naye kwenye mahusiano.

Ujumbe huo alioandika  Kajala ni huu hapa "Mfano kamili kwamba kuwa peke yako ni bora kuliko kuwa na mtu asiye sahihi/mbaya".Aandika Kajala.

Aisee tayari Harmonize ametumia njia mbalimbali kumshawishi mrembo huyo ikiwemo  kuweka bango la picha yake akiwa na Kajala maeneo ya Kinondoni, kuandika jina la Kajala kwenye gari ya kifahari, kuweka picha yake ukutani mwake yote hayo ni kutaka kumshawishi ili warudiane.

Ebwanaaa eeeh!! Unaweza kumshauri chochote Harmonize kwa kudondosha comment yako kupitia website yetu www.mwananchiscoop.co.tz.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags