Kaizer Chiefs yarudi tena kwa Nabi

Kaizer Chiefs yarudi tena kwa Nabi

‘Klabu’ ya Kaizer Chiefs imeonesha tena nia ya kutaka huduma ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi baada ya mwaka jana kumkosa.

Dili la Nabi kwenda Kaizer lilifeli baada ya kushindwana nao kwenye baadhi ya masharti kisha Molefi Ntseki kuchukua mikoba hiyo ambapo alidumu kwa miezi mitatu kabla ya kutimuliwa.

Nabi ambaye kwa sasa anaifundisha FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Julai 2023 akitokea kwa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga.

Amakhosi wamehusishwa na majina kadhaa, ikiwamo Alexandre Santos raia wa Ureno ambaye ameachana na wababe wa Angola Petro de Luanda baada ya kushinda taji la Ligi Kuu Angola.

Kaizer inaonyesha zaidi nia ya kumtaka Nabi baada ya kumkosa msimu uliopita kutokana na kushindwana kwenye baadhi ya masharti ila kwa sasa wapo tayari.

Miamba hao wa Soweto, ambao wamemaliza kampeni za msimu wa 2023/24 katika nafasi mbaya ya 10 ikiwa ni rekodi mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo, sasa wako tayari kulipa fidia kwa AS FAR ili kununua kandarasi ya Nabi ambayo inaisha Juni 2025.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post