Kagame awafuta kazi wanajeshi

Kagame awafuta kazi wanajeshi

Mkuu wa jeshi na waziri wa ulinzi nchini Rwanda wamefutwa kazi kwa wakati mmoja, hali ambayo si kawaida nchini humo ni baada Rais Paul Kagame kuchukua maamuzi hayo pasipo kutaja sababu.

Aidha uamuzi huo wa Kagame ulifuatiwa na Juvénal Marizamunda kuteuliwa kuwa waziri wa ulinzi akichukua nafasi ya meja jenerali Albert Murasira aliyeshika nafasi hiyo tangu 2018.

Kwa nafasi ya mkuu wa jeshi Rais wa nchi hiyo alimpatia Luteni jenerali Mubarakh Muganga akichukua nafasi ya generali Jean Bosco aliyeongoza idara hiyo tangu 2019.

Sambamba na hayo Rais kagame pia amewabadilisha makamanda wakuu wa wanajeshi waliotumwa msumbiji kusaidia kupambana na wanamgambo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags