Kaburi la Mama Megan kulindwa na polisi

Kaburi la Mama Megan kulindwa na polisi

Baada ya ‘rapa’ Nicki Minaj na #MeganTheeStallion kuingia katika bifu zito kuhusaina na Nicki kufanya mzaha na kaburi la mama mzazi wa Megan hatimaye inadaiwa kuwa kaburi hilo kwasasa liko katika uangalizi wa polisi.

Kwa mujibu wa TMZ, polisi wameamua kuchukua hatua ya kulinda kaburi la Marehemu mama yake ‘rapa’ #MeganTheeStallion aitwaye Holly Thomas ikiwa ni baada mashabiki wa Nicki Minaj kutaja eneo lililopo kaburi hilo na kutoa vitisho vya kufukua maiti ya Bi Holly, kupitia mitandao ya kijamii.

Bifu la wawili hao lilianza mwaka 2019 baada ya Megan kuanza kufananishwa na Nicki lakini bifu hilo limezidi kuwa zito zaidi baada ya #Megan kutoa ngoma ambayo imedaiwa kuwa aliwachana makavu ma-staa mbalimbali akiwemo Nicki hivyo basi, #Minaji hakutaka kulikalia kimya ndipo akaamua kumjibu kupitia wimbo wa ‘Big foot’ aliouachia siku ya Jumapili.

Holly Thomas (Mama Megan) alifariki mwaka 2019 baada ya kuugua saratani ya ubongo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags