Jux na mpenzi wake kumalizia bata lao Dar

Jux na mpenzi wake kumalizia bata lao Dar


Baada kuchafua mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa mwanamuziki Juma Jux na mpenzi wake mpya Priscilla Ajoke raia wa Nigeria wameamua kumalizia bata lao nchini Tanzania.

Kufuatia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha Jux akimuuliza mpenzi wake kuwa anakwenda wapi ambapo mwanadada huyo alijibu anakwenda Dar es slaam.

Mahusiano ya wawili hao yalianza mapema mwezi Agosti huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.

Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu. Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags