Jumapili ya Januari 12, 2025 mpenzi wa msanii wa muziki wa RNB, Juma Mussa 'Jux', Priscilla Ajoke Ojo ametua Tanzania akitokea kwao Nigeria na kuthibitisha anatarajia kufunga ndoa na Jux mwaka huu.
Mrembo huyo alizungumza hayo alipotua Uwanja wa Ndege Tanzania na kusema zoezi hilo la kufunga ndoa litafanyika Tanzania na Nigeria na anatamani kupata watoto wengi baada ya ndoa hiyo.
Kutokana na habari hizo njema kutoka kwa Priscilla, Mwanaspoti liliamua kumtafuta Jux ili kumpa hongera na kujua ratiba nzima ya ndoa ambapo msanii huyo ameonesha kigugumizi kuhusiana na jambo hilo.
“Any way kuhusu kufunga ndoa bana hii Mungu akijalia nitafanya hivyo, lakini kwa sasa siwezi kusema ni lini kwa sababu hivi vitu vinapangwa na familia, ndugu mkishapanga. ikishakuwa official kila mtu atajua tu
Pia hivi vitu bana kama nilivyosema huko nyuma, kutangaza tangaza ndoa ikiwa mambo hayajakamilika mwishowe itakuja kuonekana kama unawachezea wadada wa watu kwa kuingia na ahadi za kutaka kufunga nao ndoa wakati siko hivyo,” amesema Jux
Licha ya mpenzi wa mwanamuziki huyo kuweka wazi kuwa anafunga ndoa mwaka huu lakini kwa upande wa Jux ameeleza kuwa mambo yatakapokuwa tayari atatoa taarifa mwenyewe.
“Siku zote wanawake wako hivyo, na nimpongeze tu kwa ujasiri huo wa kuzungumza hilo na niseme nampenda sana ni kuomba tu kwa Mungu iwe hivyo InshaAllah.
Muda wangu ukifika mie nitaweka wazi kwasasa mniache kwanza, ila jueni anaithamini sana ndoa ikiwa mimi ni mtoto wa kiume nakusudia kupiga hatua hiyo,” amemalizia Jux.
Utakumbukwa kuwa Jux amewahi kuwa kwenye na mahusiano na mastaa mbalimbali akiwemo Vanessa Mdee, Karen huku miaka ya nyumba akihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamitandao kutoka Kenya, Huddah Monroe
Leave a Reply