Justin Bieber sasa ni baba

Justin Bieber sasa ni baba

Baada ya kutangaza kutarajia kupata mtoto miezi michache iliyopita, hatimaye mwanamuziki Justin Bieber na mke wake Hailey wamepata mtoto wao wa kwanza aitwaye Jack Blues Bieber.

Bieber amethibitisha kupata mtoto huyo siku ya jana Ijumaa Agosti 23, kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa ku-share picha ya mguu wa mtoto huku akimkaribisha nyumbani.

Aidha kupitia posti hiyo baadhi ya ma-staa kutoka nchini Marekani akiwemo Kim Kardashian na wengineo wamempongeza Bieber na mkewe kwa kupata mtoto wao wa kiume.

Ndoa ya wawili hao sasa inamiaka sita tangu walipofunga kwa siri huko New York mwaka 2018.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags